Kikaragosi dhidi ya bwana wa Vikaragosi

Blogu

Je, uliwahi kutazama filamu ya The Departed?

Kwa hiyo filamu, nikikumbuka vizuri kulikuwa an wakala fisadi wa FBI, mwenye alifanya kama kikaragosi kwa mkubwa wa Kundi la watu ( Bwana wa Vikaragosi),matokeo yake huyo mkubwa wa Hindi la watu alimtumia wakala wa FBI kutekeleza ajenda yake.

Ninakumbuka filamu hii kwa sababu niliitazama hivi karibuni kitu kuhusu ulimwengu uliojaa watu ” wenye nguvu” (bwana wa vikaragosi) ambaye hufanya kazi kwa vivuli, wakidanganya watu maarufu ( vikaragosi) kwa ajili ya kutekeleza ajenda yao maovu.

Hivyo najiuliza, vipi ikiwa ulimwengu kama huu upo tayari. Vipi ikiwa maovu mengi ya ulimwengu huu yalisababishwa na mabwana wa vikaragosi wakitumia vikaragosi kutekeleza matendo yao maovu.

Kivipi ulimwengu huu utajikomboa kutoka kwa ulimwengu uliojengwa karibu na nguvu za kivuli? Unajuaje wa kumthamini kwa ulimwengu kama huo? Ni nafasi gani vikaragosi hawa hutekeleza kwa haya yote? Je, hao wenyewe ni wanyonge au washirika?

Shida ni kuwa, katika mazingira ya kivuli ya nguvu nitadhani kuwa kikaragosi anaweza endelea kumlinda bwana wa vikaragosi ambaye ana ” nguvu halisi” kwa sababu, kikaragosi huyo anamwogopa kikweli bwana wa vikaragosi.

Kwa hivyo, ikiwa ukosefu wa ushujaa ndio msukumo wa kweli kwa vikaragosi, basi kivipi ulimwengu huo hujitenga wazi kutoka kwa kikaragosi mwoga?

Sasa, hilo ndilo swali la dhahabu,na ilinichukua muda kupata pa kuanzia, hitilafu kwenye mfumo.

Kwa kuzingatia kuwa wema daima hushinda uovu,ni jambo lisiloepukika kwamba dirisha dogo la fursa litatokea kila wakati, kama mwanzo wa ulimwengu huu. Hali inayofaa kwa kishindo kikubwa.

Lakini fursa hii inaweza kuwa nini?
Naam, hebu turudi kwenye mojawapo ya sababu zinazowafanya vikaragosi kuweza kunaswa kwa mfumo huu, ukosefu wa ushujaa.

Kwa kuzingatia hii, fursa hiyo inaweza kutokea wakati kwa sababu fulani kikaragosi yule anahitaji kukataliwa na huyo bwana wa vikaragosi kwani kikaragosi angeweza kwa namna fulani kujifanya kuwa hatari kwa shirika.

Katika hali hii, kikaragosi huyo angewekwa chini ya uchunguzi wa kiwango ambacho hawakuahi stahimili hapo awali kwani walikuwa na ulinzi wa bwana wa vikaragosi awali.

Sasa kikaragosi kwa mara ya kwanza anajikuta kati ya mwamba na mahali pagumu. Utafanya nini ikiwa ulikuwa huyo kikaragosi? Kutofanya jambo litamaanisha kikaragosi huyo pamoja na familia yake watabeba mzigo mkubwa wa haki ya watu kutokana na uhalifu uliofanywa kwa niaba ya shirika ambalo lilimsaliti tu. Kingekuwa nini la kududi ya maisha ya kikaragosi huyo?

Chaguo linalofaa kwa kikaragosi anayejuta ni kufichua bwana wake. Kwa matokeo yake, kutuma ujumbe kwa umma kuwa yule kikaragosi hataki tena kuwa moja wa shirika lile ovu. Uwe na uhakika kuwa umma utakuwa wa haki kwa kikaragosi na familia yake, kuliko chaguo mbadala ya kuwa chini ya utumwa wa kikaragosi mwovu.

Angalau kwa chaguo hili,historia na umma kwa jumla utatambua kuwa kikaragosi alikuwa sehemu ya chombo kilichomwangusha bwana wa vikaragosi kama tu Daudi dhidi ya Goliathi.

Baada ya kusema haya, ni rahisi kusema kuliko kufanya. Kusaliti bwana wa vikaragosi,kisaikolojia, huenda isiwe rahisi kwa sababu ukweli ni kwamba kikaragosi anaogopa na ndivyo ilivyokuwa maisha yote ya kikaragosi. Zaidi ya hayo, vikaragosi wengine wanawezamgeuka huyu kikaragosi kwa sababu hao pia wanaogopa.

Hii ndiyo maana ninaamini inahitaji hali fulani ili kumwangusha bwana mbaya wa vikaragosi. Kwa mfano, mazingira ambapo idadi kubwa ya vikaragosi hawafurahishwi na bwana yao na wanataka tu kujinasua na kutumia maisha yao kwa manufaa makubwa ya ubinadamu.

Kwa muhtasari, kama kikaragosi anayetupwa nje ya shirika ambalo linamlinda kila wakati, ungemwamini nani? Ni bwana mbaya wa vikaragosi? Au maadili yako. Ni urithi gani ungewaachia wapendwa wako, ulimwengu mzuri au mbaya.

Ikiwa hauamini, kumbuka, ukweli utakuweka huru.

Ikiwa unapenda nakala hii unaweza kupenda pia onyesho la sanaa NI ALBAMU YA RAP na Ufunuo, Inuka, Tawala. zinajumuisha vipande kama vile #Kunguni, #Watumwa_Wanaojifanya_Ku wa_Wafalme na #Teknolojia_Ya_Huawei_yenye _ubunifu #5G_6G

Sisi ni Nyeusi. Ujumbe uko wazi. Nyeungana.

Nyeusi ni shirika la hisani ambalo lengo lake ni kujenga upya jamii ya watu weusi, maono yetu ni Nyeungana. Ifa Dudu dada yetu kampuni ya hisani ni dini inayozingatia maono ya Nyeungana.

Utufuate kwenye mitandao ya kijamii,jiandikishe kwa jarida letu na ushiriki nakala hii ikiwa unamfahamu mtu ambaye angeipenda.

Pia shiriki mawazo yako hapa chini tafadhali

r

Kanusho la Maoni: Hii ni blogu na imewasilishwa jinsi ilivyo. Mapendekezo yoyote, madai au hoja yoyote yaliyotolewa yanawasilishwa kama maoni tu. Haifanyi madai yoyote kuwa ya kweli, ya kisayansi, au ya kisheria kwa njia yoyote.

 

 

Pitisha chapisho hili: